WATANZANIA TUJIANDAE! Yaliyotokea Morogoro Dhahiri Mwisho Wa Dunia Umefika Tazama
Katika hali isiyo ya kawaida imeibuka katika Manispaa ya Morogoro baada ya mwanaume mmoja aliyedaiwa kupotea mwaka 2022 leo mabaki yake yamepatikana na kuwaacha midomo wazi wananchi wa eneo la mtaa wa Kampani Tanu kwa huzuni na vilio.
Mabaki hayo ya mwili wa mwanaume huyo aliyekuwa anajulikana kwa jina la Christome Simon aliyekuwa na umri wa miaka arobaini na saba (47) alikiwa anaishi mtaa wa Kampani Tanu katika Manispaa ya Morogoro. Bw. Christome alitoweka mwezi wa kumi na moja mwaka jana (2022), na leo mabaki yake yamepatikana katika pori la Mgulu wa Ndege lililopo mkoani Morogoro.
Akizungumza kaka wa marehemu, Joachim Simon amesema mdogo wake alipotea katika mazingira ya kutatanisha kwani mara ya mwisho alionekana mtaani akiwa amevaa begi, baada ya hapo hakupatikana licha ya kupimgia simu yake na kumtafuta sehemu mbalimbali lakini hawakuweza kumpata na amedai kuwa hakuwa na ugomvi wala mgogoro na mtu yeyote.
Ameongezea kwa kusema alipata taarifa kuwa kuna mabaki ya mtu mmoja yameonekana kwenye pori la Mgulu, alipokwenda kufanya uchunguzi aligundua ni ndugu yake kwa kupitia simu yake, nguo na viatu alivyokuwa amevaa mara ya mwisho.
Comments
Post a Comment