Nyie Diamond Na Zuchu Wametupiga Na Kitu Kizito, Oneni Mabusu Na Mahaba Hadharani(+Video)

 

Waungwana wanakuambia Lisemwalo lipo na kama halipo bhasi Laja...! Kauli hii inanipeleka moja kwa moja hadi WCB pale Usafini kwa kaka mkubwa Diamond Platnumz na Bibie Zuhura.


Ni muda sasa umepita tangu tuanze kusikia Fununu za wawili hawa kutoka kimapenzi, na kitu kikubwa kinachokuja kuaminisha watu ni zile kauli za watu walio karibu na Familia hii ya Wasafi kupitia mahojiano mbalimbali hata comments zao pia kwenye mitandao ya Kijamii.


Hivi nani yupo wa kupinga mahusiano ya Simba na Zuchu?, Nani ambaye ana kikwazo juu ya wawili hawa endapo wakifunga ndoa. Ushawahi kufuatilia ukweli juu ya usemi usemao " Kelele za Chura hazimzuii Tembo Kunywa maji" endapo mahusiano ya Zuchu na Platnumz yatakuwa yanakukera ilihali mtu kama Mama Dangote, Esma, Romy Jones, Don Fumbwe na Kina Lokole wamempitisha binti huyu wa kizanzibar we ni nani hadi ueleweke kwa Mond?.


Nadhani ni Muda sahihi sana kwa Simba kutulia na Kufunga ndoa na Binti huyu, kwanza wanaendana sio tuu kwenye Collabo za ngoma walizowahi kuzitoa, No hata kwenye picha hapo wawili hawa wamependeza mnoo nadhani hata huko. kwingine pia wanaendana bila shaka. 


Sasa basi mapenzi yao Yamezidi kudhurika katika tukio la usiku wa kuamkia leo katika Ukumbi wa Mlimani City kulikuwa na tukio kubwa ya harusi ya mfanyakazi wa Wasafi Don Fumbwe. Harusi ilikuwa ya Don lakini mtandao ni kelele za Zuchu na Diamond wakiwa ndani ya Ukumbi. Na kuna mengi wamefanyika usiku huo kwa wawili hao.


Hii leo Diamond na Zuchu wameamua rasmi kuweka wazi kuwa wako sahihi na si kweli kwa maneno yanayoendelea kwenye mitandao. Wawili hao wameonekana wakibusiana na kuwa karibu kila mara, katika sherehe hiyo. Kitendo cha Zuchu kinaonekana kuganda kwa Chibu, baadhi ya watu wamekuwa na mitazamo tofauti, hasa wengi wenye mitazamo hasi juu ya Zuchu kuwa karibu na kutoka kimapenzi na Diamond ambaye ni Boss wake.

Comments